Tumia iPhone yako kubaini ikiwa kitu kilicho karibu nawe ni cha kiwango, kimenyooka au tambarare (vipimo ni vya kukadiria).

- Fungua Kipimo.
- Gusa Kiwango, kisha ushikilie iPhone dhidi ya kitu, kama vile fremu ya picha.
- Tengeneza kiwango cha kitu: Zungusha kipengee na iPhone hadi uone kijani.
- Linganisha mteremko: Gusa skrini ili kunasa mteremko wa kitu cha kwanza. Shikilia iPhone dhidi ya kitu kingine na uzungushe hadi skrini igeuke kijani.
Ili kuweka upya kiwango, gusa skrini tena.